Kumb. Na EA.7/96/01/H/67 15 Septemba, 2015
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho
kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002
kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa
mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa
jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa
Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya
waajiri mbalimbali Serikalini anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye
sifa na uwezo wa kujaza nafasi 120 za kazi kama zilivyorodheshwa katika
tangazo hili.
1.0 AFISA MTENDAJI WA KATA DARAJA LA II (WARD EXECUTIVE OFFICER GRADE II) – NAFASI 20
1.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Atakuwa Mtendaji Mkuu wa Kata na kiungo cha Uongozi kwa Idara zote katika kata na atashughulikia masuala yote ya kata
• Atakuwa Mhamasishaji mkuu wa Umma katika mikakati mbalimbal.i ya uzalishaji,
mali, kuondoa njaa na Umasikini.
• Atakuwa ni Katibu wa kamati ya maendeleo ya kata.
• Ataratibu na kusimamia upangaji wa shughuli za maendeleo ya kata, vijiji na Mtaa.
• Atatafsiri
sera na kusimamia utekelezaji wa sheria ndogondogo katika Kata
yake.Atamsaidia Mkurugenzi Kuratibu na kusimamia shughuli za Uchaguzi
katika Kata.
• Kumsaidia na kumwakilisha Mkurugenzi katika kusimamia maendeleo ya eneo lake.
• Kusimamia utendaji kazi wa wataalamu na watendaji wengine katikangazi ya Kata.
• Kuratibu na kuandaa taarifa za utekelezaji na kuziwasilisha kwa mkurugenzi na nakala kwa Katibu Tarafa.
• Atakuwa mwenyekiti katika vikao vinavyowahusisha wataalamu na watendaji wa vjiji, na NGO’S katika kata yake.
• Atakuwa Msimamizi na mratibu wa takwimu zote zinazokusanywa katika vijiji, vitongoji, na kata yake.
1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya Juu katika fani ya Utawala, (Public
Administration and Local Gorvernment), Rasiliamaliwatu, Sheria, Elimu ya Jamii,
Maendeleo ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Uchumi na Mipango
kinachotambuliwa na Serikali.
1.3 MSHAHARA
• Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D. kwa mwezi.
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji
ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya
nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Waombaji
waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini
(referees)
watatu wa kuaminika.
v. Maombi
yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya
kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na
vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi
husika.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni.
vi. Testmonials”,
“Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato
cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA.
vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix. Waombaji
kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko
katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo
yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xi. Mwisho wa maombi ni tarehe 29 Septemba, 2015
xii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xiii. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa
Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo;
http://portal.ajira.go.tz/
(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)
xiv. MUHIMU:
KUMBUKA KUWEKA (ATTACH) BARUA YAKO YA MAOMBI. ANUANI YA BARUA HIYO
IELEKEZWE KWA KATIBU, OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA
UTUMISHI WA UMMA S.L.P 63100 DAR ES SALAAM.
Thursday, September 17, 2015
AFISA MTENDAJI WA KATA (WARD EXECUTIVE OFFICER )
By writer at 10:07 AM
job-government
Related Posts:
KUITWA KWENYE USAILI , Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania - OKT 2015 TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania inawatangazia wale wote waliofanya usaili wa mchujo (written interview) tarehe 12 – 14 Agosti 2015 na 7 – 8 Septemba 2015 kwa nafasi za Afisa Udahili Daraja la II… Read More
TAARIFA KUHUSU AJIRA ZA MAGEREZA Jeshi la Magereza nchini limetoa taarifa ifuatayo, kukanusha taarifa za tangazo la ajira katika Jeshi hilo ambayo imekuwa ikisambazwa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii hivyo kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi na … Read More
KUITWA KWENYE USAILI , Tume ya Utumishi wa Mahakama - OKT 2015 KUITWA KWENYE USAILI Tume ya Utumishi wa Mahakama inawatangazia watu wote walioomba kazi za kada mbalimbali kuwa wameteuliwa kuhudhuria usaili wa kazi walizoomba utakaofanyika kwenye kumbi zilizoko ndani ya uwanja wa Tai… Read More
Nafasi za Kazi Manispaa ya Ilala , Okt 1 2015 Msimamizi wa Uchaguzi Manispaa ya Ilala anawatangazia wananchi/Wakazi wote wa Manispaa ya Ilala Nafasi Zifuatazo 1.Wasimamizi wa Uchaguzi wa Vituo 2. Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo 3.Makarani Waongozaji wa Kupiga Kura Sifa … Read More
Deputy Executive Secretary , Tanzania Commission for Universities (TCU) The Tanzania Commission for Universities (TCU) is a semi-autonomous statutory body under the Ministry of Education and Vocational Training. TCU is mandated to recognize, approve, register and accredit universities operat… Read More