Kumb. Na EA.7/96/01/H/67 15 Septemba, 2015
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho
kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002
kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa
mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa
jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa
Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya
waajiri mbalimbali Serikalini anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye
sifa na uwezo wa kujaza nafasi 120 za kazi kama zilivyorodheshwa katika
tangazo hili.
3.0 AFISA KILIMO MSAIDIZI DARAJA LA III (AGRICULTURAL FIELD OFFICERS)
– NAFASI 20
3.1 MAJUKUMU YA KAZI.
• Kushirikiana na wakulima kuendesha mashamba ya majaribio na mashamba darasa,
• Kutembelea
wakulima/vikundi vya wakulima katika mashamba yao na kutoa ushauri wa
kitaalamu juu ya mbinu bora na za kisasa za kilimo cha kibiashara,
• Kufundisha na kuelekeza wakulima juu ya matumizi bora ya mbolea, madawa na zana za kilimo,
• Kukusanya na kutunza takwimu za hali ya kilimo katika kijiji,
• Kubuni na kuandaa vihenge vya kisasa vya hifadhi ya mazao na kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mazao,
• Kutoa taarifa juu ya dalili za kuwepo visumbufu vya mimea na mazao,
• Kuandaa na kutumia daftari la kilimo katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku,
• Kushiriki
katika mchakato wa kuibua fursa na vikwazo vya maendeleo (Opportunities
and Obstacles for Development (O & OD) na kuandaa mpango wa
maendeleo ya kilimo wa kijiji (Village Agricultural Development Plan
(VADP), na
• Kuandaa
taarifa ya utekelezaji ya kila mwezi kuiwasilisha kwa Afisa Ugani wa
Kata na nakala kuiwasilisha kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji.
3.2 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa waliohitimu kidato cha nne wenye Astashahada (Cheti) ya Kilimo
kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
3.3 MSHAHARA
• Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS B Kwa
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji
ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya
nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Waombaji
waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini
(referees)
watatu wa kuaminika.
v. Maombi
yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya
kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na
vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi
husika.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni.
vi. Testmonials”,
“Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato
cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA.
vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix. Waombaji
kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko
katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo
yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xi. Mwisho wa maombi ni tarehe 29 Septemba, 2015
xii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xiii. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa
Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo;
http://portal.ajira.go.tz/
(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)
xiv. MUHIMU:
KUMBUKA KUWEKA (ATTACH) BARUA YAKO YA MAOMBI. ANUANI YA BARUA HIYO
IELEKEZWE KWA KATIBU, OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA
UTUMISHI WA UMMA S.L.P 63100 DAR ES SALAAM.